Wazalishaji wa bidhaa za ngozi washauriwa kuwekeza kwenye sekta ya ngozi ili kujipanua kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi kutokana na uhitaji mkubwa uliopo wa bidhaa za ngozi.
Hayo yalisemwa na Prof Adolf Mkenda Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji), akiyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa wazalishaji wa bidhaa za ngozi uliofanyika tarehe 15 Septemba, 2016 kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl. J.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
“Serikali imedhamiria kuiwezesha sekta binafsi kuanzisha viwanda ili kukuza bidhaa za Tanzania ikiwemo bidhaa za sekta za ngozi, hivyo washiriki wa mkutano huo waliaswa kutumia fursa kuzidisha bidhaa bora na ushindani”
Aidha, Prof Mkenda alitumia muda huo kuwahamashisha wazalishaji hao kutumia soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na soko la SADC. Na pia kuitumia TanTrade pamoja na taasisi zingine za Serikali zinazoweza kuwainua kwenye sekta hiyo ili kuondokana na changamoto zinazokabili sekta hiyo.
Naye, Bw Edwin Rutageruka Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), aliwaambia wazalishaji hao kuwa TanTrade ipo tayari kuwapa mafunzo ya ujasiliamali wa namna watakavyoweza kupenya kwenye masoko mbalimbali ili kukuza sekta hiyo ya ngozi
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ilishirikiana kuandaa mkutano wa wazalishaji wa bidhaa za ngozi ikiwa na lengo la kuwakutanisha wadau wa Serikali na sekta binafsi ili kujadili fursa, changamoto na mikakati ya kuendeleza sekta hiyo ambayo inamchango mkubwa katika ukuaji wa sekta ya viwanda na uchumi nchini. Sambamba na mkutano huo maonesho madogo ya bidhaa za ngozi yalifanyika ambapo wazalishaji wapatao 63 walionesha bidhaa zao mbalimbali.
Leather Economic Sub-Sector
TAARIFA ZA BIASHARA
Bonyeza hapa chini kupakua Taarifa za Biashara
Fomu ya Maombi ya Taarifa za Biashara (Information Request Form)
General Procurement Notice 2017/2018
Click here to download General Procurement Notice
EXHIBITION CALENDER 2018 Download
TRADE FAIR/EXHIBITION IN TANZANIA
TERMS FOR ORGANIZERS OF INTERNATIONAL TRADE FAIRS IN TANZANIA
Click here to download TOR for Trade Fair Organisers
Click here to download an Application Form for Authorization